WAKULIMA WA KOROSHO WAIPA KONGOLE SERIKALI.

Kilwa,

Wakulima wa zao la korosho wilayani Kilwa wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa jitihada inayoendelea kuonyesha katika kuhakikisha zao la korosho linawaingizia kipato kikubwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Shukrani hizo zimetolewa na Makamu Mweneyekiti wa Chama cha msingi umoja Mikoma Mohamedi Hassan Ally alipokua akizungumza na waandishi wa habari za vijijini walipofika kjijini hapo kujionea shughuli na changamoto mbalimbali amabazo zinazowakabili wakulima hao.

Bw. Mohamedi amesema maboresho katika mfumo wa stakabadhi ghalani umewasaidia sana kwani kwa sasa mkulima analipwa kwa mkupuo stahiki zao zote baada ya mnada tofauti na zamani ambapo mkulima alikua analipwa kwa awamu hali ambayo ilikua inawapelekea kuuza korosho zao kwa walanguzi (Chomachoma) kwa bei ya kutupwa.

“tunaishukuru sana kwa maboresho haya katika utaratibu huu wa mauzo kwani sasa tunapata stahiki zetu zote kwa mkupuo na kwa wakati tofauti na zamani ambapo tulikua tunalipwa kwa awamu” alisema Mohamedi

Aidha Bw. Mohamedi ameiomba serikali kuwahisha pembejeo ili waweze kupulizia mikorosho kwa wakati ili kupata mazao mengi yakiwa katika ubora unaotakiwa.

“msimu huu wamegawa salfa kwa ajili ya kupulizia mikorosho lakini haikua nyingi na ilichelewa kidogo kwahiyo tunaomba waongeze kiasi cha pembejeo na ifike kwa wakati .” alisisitiza bw, Mohamedi
Makamu Mweneyekiti wa Chama cha msingi umoja Mikoma Mohamedi Hassan Ally akizungumza na Muandishi wa habari za vijijini Bi. Pamela Mollel baada ya kufika  kjijini  hapo kujionea  shughuli na changamoto mbalimbali amabazo  zinazowakabili wakulima wa zao la korosho.(picha na Ally Ruambo)
Nae mkuu wa wilaya ya Kilwa Mh. Cristopher Ngubiagai amesema serikali iko makini juu ya walanguzi (chomachoma) ambao watajaribu kununua korosho kinyume na utaratibu na kuahidi kuchukua hatua kaili za kisheria ikiwa pamoja na kutaifishwa kwa mzigo ambao utakamatwa.

“endapo chomachoma atakamatwa ananunua korosho kinyume na utaratibu, tutataifisha mzigo wote, tutamkamata mwenyeji wake na sehemu ambayo atakua anahifadhia korosho zake baada ya kulangua na hatua zingine kali za kisheria zitafuata dhidi yake.” Alisisitiza Mh. Ngubiagai

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai akizungumza na waandishi wa habari za vijijini walipomtembelea ofisini kwake. (picha na Ally Ruambo)
Mh. Ngubiagai amesema kamati ya ulinzi na usalama ipo makini kuhakikisha hakuna udanganyifu au utoroshwaji wowote wa korosho ambao utafanyika.

Pia mh. Ngubiagai ameahidi kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha pembejeo zinapatiakana kwa wingi zaidi ya msimu uliopita na kwa wakati muafaka sambamba na kuhakikisha korosho zinanunuliwa kwa bei yenye manufaa kwa wakulima na kuwataka wakulima kulima kilimo cha tija na manufaa.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo amesema halmashauri ya wilaya ya Kilwa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka idara ya kilimo inaotesha miche milioni moja ya mikorosho ambayo itagawiwa bure kwa wakulima ikiwa ni jitihada za kukuza na kuongeza pato la halmashauri kupitia zao la korosho.

Bw. Bugingo amesema zoezi la uoteshaji wa miche ni zoezi endelevu ambalo litakua linafanyika kila mwaka.

Katika msimu wa 2016/2017 zao la korosho liliingizia halmashauri zaidi ya shilingi bilioni kumi na tatu ambapo baada ya mgawanyo halmashauri ya wilaya ya kilwa ilipata zaidi ya milioni 200.
Previous
Next Post »