Kundi la Friends of mnazi mmoja wameitembelea shule ya msingi mnazi mmoja iliyopo wilayani kilwa na kufanya mazungumzo na walimu wa shule hiyo kuhusu mambo mbalimbali ambayo yataisaidia shule ya msingi Mnazi mmoja na sekta ya elimu kwa ujumla.
Pia wamekabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi Laki moja na kumi kwa uongozi wa shule hio ikiwa nijitihada za kuunga mkono mradi wa ufugaji kuku unaotarajiwa kuanzishwa ana shule hio kwa lengo la kujiongezea kipato na elimu ya kujitegemea (Ek) shuleni hapo.
Friends of Mnazi mmoja ni kikundi ambacho kinaundwa na wahitimu wa Shule ya msingi mnazi mmoja katika miaka tofauti.
| Muweka hazina wa Friends of mnazi mmoja Nd.Songolo Lilacho akikabidhi mchango kwa uongozi wa shule ya msingi mnazi mmoja , kushoto ni Hamisi Kassinge mratibu wa tukio. |
| Friends of mnazi mmoja katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi mnazi mmoja ( Picha na Ally Ruambo) |
| wawakilishi wa Friends of Mnazi mmoja katika picha ya pamoja. |
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon