Mkuu wa wilaya ya Kilwa
mhe. Cristopher Ngubiagai (katikati)
na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo (wa kwanza kulia) wakimsikiliza moja ya wadai
baada ya mkutano uliofanyika tarehe 19 mwezi huu katika kijiji cha Lihimalyao.
Mkutano huo ulifanyika
baada ya kupokea taarifa ya baadhi ya wakulima wa zao la korosho kufunga ghala la kuhifadhia korosho kijijini
hapo wakishinikiza kulipwa madai yao
yaliyotokana na uuzwaji wa korosho zao msimu uliopita.
Akiambatana na kamati
ya ulinzi na usalama mkuu wa wilaya aliwasihi wananchi kuacha kujichukulia
sheria mkononi kwani kwa kufanya hivyo wanakua wanaenda kinyume na sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha mkuu wa wilaya
amewaomba wananchi ambao wanadai stahiki zao waendelee kua na subira kwani
wanatambua kua wananchi hao wanadai na serikali iko macho kuhakikisha inawasaidia wakulima hao kupata stahiki
zao haraka iwezekanavyo.
Katika mkutano huo watu
kadhaa walikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kushiriki katika mchakato wa kufunga ghala hilo na kuzuia
wakulima wengine kuhifadhi korosho zao kwa ajili ya mauzo hali iliyopelekea kuhatarisha usalama wa mazao yao.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon