MTIBWA SUGAR YAICHAPA BLACK MOB FC 3-1



Mabingwa watetezi wa mshikamano cup, Black mob fc kutoka  mji kingunge wa Kilwa kivinje imekubali kipigo cha goli tatu kwa moja kutoka kwa Mtibwa sugar wana tamu tamu katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo novemba sita katika dimba la ukote mjini Kilwa kivinje.

Mchezo  huo wa kukata na shoka umepigwa kwa dhumuni la kutoa burudani kwa wepenzi wa soka wilayani Kilwa sambamba na kuonyesha vipaji ambavyo vinapatikana Kilwa huku mtibwa sugar wakiutumia mchezo huo kama kipimo  kuelekea mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya ndugu zao wakata miwa Kagera sugar.

timu zote zilionekana kuanza mtanange kwa kucheza mchezo wa kujihami  na  kushambuliana kwa zamu  kabla ya mkongwe Henry Joseph Shindika kukata utepe wa magoli kwa kuiandika timu yake ya mtibwa sugar bao safi la kuongoza katika dakika ya Thelathini na nane ya mchezo baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa kutoka magharibi ya uwanja.

Mpaka timu zinakwenda mapumziko mtibwa sugar ilikua mbele kwa goli moja dhidi ya wapinzani wao.


Dakika kumi na nne mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili mchezaji Kelvin Sabato akaifungia mtibwa goli la pili katika mtanange huo na kufanya ubao usomeke goli mbili kwa mtibwa na sifuri kwa wenyeji.

Kelvin sabato aliendelea kuli didimiza jahazi la Black mob fc kwa kufunga goli la tatu kwa mtibwa sugar na la pili kwake katika mtanange  huo katika dakika ya sitini na saba ya mchezo.

Zikiwa zimesalia dakika kadhaa Black mob fc walifanya mabadiliko ya kiufundi na kuwaingiza wachezaji wawili kwa pamoja, wachezaji ambao walisaidia kubadili mchezo na kufanikisha kupata bao la kufutia machozi lililo wekwa wavuni na Anderson Rage katika dakika ya Themanini na tatu ya mchezo kwa shuti kali lililo mshinda mlinda lango wa mtibwa.

Black mob fc walionekana kuchachamaa katika dakika za lala salama mara baada ya kuonja ladha ya goli kwa kulisakama goli la mtibwa bila mafanikio.

Mpaka muamuzi Ahmadi tiwa anapuliza kipyenga kuashiria kumalizika kwa pambano hilo mtibwa sugar tatu black mob fc moja.


Baadaya mchezo huo mundunkolo.blogspot ili bahatika kufanya mahojiano na golikipa namba moja wa mtibwa sugar Benedict Tinoco alisema

“Tunashukuru mungu mchezo umeisha salama na tumepata changamoto ya kutosha kuelekea mchezo wetu wa ligi kuu dhidi ya kagera sugar katika uwanja wa nyumbani, na pia nawashauri ndugu zangu wafuate miiko ya soka watafika mbali kwani vipaji wanavyo vya kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu.


Akiwakilisha timu ya black mob fc mchezaji Juma Jega amewashukuru waandaji wa mechi kuanzia ile ya Lipuli, Ndanda na ya Mtibwa pia amewataka wachezaji amba bado hawajatoka kutumia mechi hizo kama funzo kwao ili waweze kufikia malengo waliojiwekea kupitia soka.

Mtibwa imesafiri kuelekea morogoro ikiwa imecheza michezo mitatu ikiwa kusini mwa Tanzania ukiwemo mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda fc, na michezo miwili ya kirafiki. 
 picha zote na Ally Ruambo.

Latest
Previous
Next Post »