Kilwa,
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amewataka viongozi
wa serikali wilayani Kilwa Mkoani Lindi kuhakikisha wanasimamia vyema upandaji
wa miche mipya yazao la korosho hali ambayo itaongeza uzalishaji wa zao hilo
kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa
Hayo aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya
kuelezwa kuwa mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda
miche milioni moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka
laki sita yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu.
| Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kulia ni Mkuu wa wilaya ya kilwa Christopher Ngubiagai (picha na Pamela Mollel,Kilwa) |
Kufuatia hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na
kustawi lazima uwepo usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani
humo kuliko kuacha usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha
kukauka na kushindwa kufikia malengo
Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo alisema tayari
hatua za awali za kuotesha miche milioni moja kila mwaka zinaendelea ambazo
miche hizo itagawiwa bure kwa wakulima hali ambayo itainua uchumi wao.
Bugingo alisema mpango huo ni wakudumu ambapo kila mwaka wilaya
itazalisha miche hiyo milioni moja na kuigawa kwa wakulima bure hali ambayo
itakuwa zaidi ya mara mbili ya uzalishaji wa miche iliyopo ambayo kwa sasa ni
laki sita tu iliyowaingizia shilingi Bilioni 13 na halmashauri kujipatia zaidi
ya shilingi milioni220.
Afisa
kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto akitoa taarifa ya
mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya
Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo.
Aliongeza kuwa mbali na kujipatia fedha kwa wakulima pia halmashauri
itajiongezea mapato ya ushuru baada ya serikali kufuta baadhai ya vyanzo ikiwemo
ya mabango iliyorudishwa serikali kuu hivyo zao hilo la korosho linaweza
kuingizia halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mpango huo kuwa
zaidi ya mara mbili zaidi.
Mbali na hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa
miche hiyo milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya
kupanda miche elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa
kilimo na ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John
Mkinga amesema changamoto iliyopo ni ucheleweshwaji wa mbegu hali
inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo kwenda taratibu ingawa Kakunda
amesema atawasiliana na wizara ya kilimo kumaliza tatizo hilo.
Sign up here with your email

ConversionConversion EmoticonEmoticon