MKURUGENZI NA MADIWANI WAITEMBELEA NANGURUKURU.



Kilwa,
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo akiambatana na Baraza la madiwani na watalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kilwa wamefanya ziara katika eneo linalotarajiwa kujengwa kituo cha mabasi katika kjiji cha Nangurukuru.

Dhumuni la ziara hio ikiwa ni kujiridhisha juu ya umiliki na uhalali wa wamiliki wa eneo hilo ambao wanatarajiwa kulipwa fidia baada ya tathimini ili kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi katika eneo hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo (mwenye suti nyeusi) akipitia baadhi ya vielelezo vya mmoja wa wananchi waliojitokeza kuhakikiwa maeneo yao. ( Picha na Ally Ruambo)
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Bw. Bugingo wamewataka wananchi wote ambao wamehakikiwa katika uhakiki uliofanyika kuwasilisha vielelezo vyao vyote ambavyo vinaonyesha uhalali wa umiliki wa maeneo hayo katika ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa siku ya tarehe saba mwezi wa kumi na moja (07/11/2017) kwa ajili ya kujiridhisha na kuendelea na hatua inayofuata.

Previous
Next Post »