MATUKIO KATIKA PICHA.

PICHA 1.    Mkuu wa shule, Shule ya sekondari Kilwa Bw. Kashaija (Katikati) akisoma risala kwa Wajumbe wa ALAT mkoa wa Lindi na Watalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa walipo tembelea shuleni hapo  tarehe 17 mwezi wa 8 kujionea shughuli za ujenzi wa majengo kadhaa yakiwemo mabweni 2 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 180. Kutoka kushoto Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Lindi  Mh. Rashidi Nakumbya , kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Nd. Zablon I. Bugingo.
PICHA 2.   Afisa mipango Wilaya ya Kilwa Bw. Kaunda (kushoto) akijibu maswali kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Justin J. Monko alipotembelea Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali.
PICHA 3.  Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Lindi Mh. Rashidi Nakumbya (Kulia) akipokea maelezo kutoka kwa aliyekua Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhandisi Chande walipotembelea shule ya msingi tingi tarehe 17 mwezi wa 8 mwaka 2017.
PICHA 4.  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tingi wakiwa na nyuso za furaha baada ya kutembelewa na Wajumbe wa ALAT shuleni hapo. Wakiwa katika Shule ya Msingi Tingi wajumbe wa ALAT na wataalamu mbalimbali walishuhudia majengo mbalimbali ikiwemo vyoo ambayo vimekamilika na vako tayari kwa matumizi.


PICHA 5. Moja ya matanki makubwa yanayopatikana katika mradi mkubwa wa maji Mingumbi – Miteja, mradi ambao ulitembelewa na wajumbe wa ALAT na kujionea jinsi unavyofanya kazi tarehe 17 mwezi 8 mwaka 2017.
Mradi wa maji Mingumbi-Miteja unatoa huduma ya maji safi na salama kwa vijiji sita ambavyo ni Kililima, Naipuli, Tingi, Mtandango, Miteja na Mingumbi yenyewe, vyenye jumla ya watu 18,120 kutoka katika kaya 3,624.
Kupitia mradi wa maji Mingumbi-Miteja upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka kwa asilimia 10% kutoka asilimia 48.3% mpaka asilimia 58.3%  kufikia juni mwaka huu.
Previous
Next Post »