PAINTER'S LOVE NI BONGE LA SIMULIZI.

Painter's Love ni simulizi ya kusisimua kutoka kwa  Shamuma Awadhi, muandishi ambae anakuja juu katika tasnia ya Uandishi.

Mundunkolo.Blogspot.com inakuletea simulizi ya Painter's Love ikiwa ni mwanzo tu wa simulizi mbalimbali ambazo zitakujia siku za karibuni kutoka kwa waandishi mahiri katika taaluma ya uandishi.

Jina la hadithi: Painter's Love
Mwandishi: Shamuma Awadhi




Ni hali isiyo ya kawaida kabisa kwa Wanafunzi Wa chuo kikuu cha Dodoma kuwepo mbele ya ofisi ya Profesa asubuhi tu baada ya kuwasili chuoni hapo. Kila mwanachuo alionekana na bango mkononi lililoandikwa malalamiko yake,Nia kubwa ya wao kugoma ni kutokana na mambo machafu ayafanyayo Profesa maziku kwa watoto Wa kike chuoni hapo.

Wasichana walikua hawana amani kabisa kwasabab ya profesa Maziku kwani akimuhitaji msichana kimapenzi lazima atampata kwa njia yoyote ile na ikishindikana anamtafutia sababu anamfukuza na kumfanyia kitendo cha kinyama hali iliyopelekea wasichana wengi kupoteza Maisha kwasabab ya kuepuka aibu na fedheha hiyo.

Na kama msichana Huyo anamchumba chuoni hapo basi mchumba wake ni lazima atafelishwa katika mitihani yake na kutumiwa watu wampige. Baada ya wanachuo hao kuchoshwa na tabia hiyo iliwabidi wagome na waende kumshitaki makao makuu ya chuo hicho.

Mtu mmoja wapo ambae ambaye alikua hatarin kufanyiwa vitendo hivyo ni kijana Derrick kipenzi cha watu wengi chuoni hapo,alitaka kufanyiwa kitendo hicho kwasabab alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti msichana mrembo sana aliyeitwa Betha ambaye pia alikua anapendwa na Profesa Maziku.


Hali ya wasiwasi ilimjaa kijana Derrick kwasabab alishawahi kuitwa kama mara mbili hivi kuonywa juu ya uhusiano wake na Betha lakini alibisha uku akiwa na wasiwasi sana,kwahyo mgomo huo uliokoa maisha yake kwa kiasi kikubwa sana.Mpaka saa nne asubuhi Profesa Maziku alikua bado hajafika chuoni hapo kwasabab alishapewa taarifa kuwa kuna hali ya hatari chuoni dhidi yake.Vikosi mbalimbali vya Ulinzi na Usalama viliwasili chuoni hapo kwaajili ya kutuliza vurugu na kuweka Usalama katika eneo hilo.

 Wanachuo hao hawakuharibu kitu chochote kwasabab mali za chuo hawakua na shida nazo,shida yao kubwa ilikua ni Profesa na si vinginevyo.Mida ya saa saba mchana Profesa Maziku aliwasili chuoni hapo akiwa na pingu mkononi uku akisindikizwa na polosi mbele,kati na nyuma ili kuweza kuhakikish Usalama wake kwasabab wanachuo walikua na hasira nae sana kiasi kwamba wasingemlinda angeweza hata kuuliwa kwa kupigwa na mawe,magongo au vitu vyenye ncha Kali.

Baada ya kuwasili alipelekwa moja kwa moja hadi ofisini kwake ambako walifanya mahojiano na waandishi Wa habari huku akiwa chini ya Ulinzi mkali. Walichaguliwa wanafunzi 5 ili waweze kuwawakilisha wenzao ambapo waliweza kumuuliza maswali na kutoa ushuhuda Wa matukio mbalimbali aliyowahi kuyafanya kwa wanafunzi wenzao.

 Katika maswali yoote waliyomuhoji Profesa Maziku hakuongea uongo hata kidogo Bali aliongea ukweli mtupu na alimaliza kwa kuwaomba wanafunzi hao msamaha kwaniaba ya wenzao,na yupo Tayari kwenda Jela.

Mahojiano yalichukua dakika arobaini na tano tu na safar ya kwenda kituoni ilianza,Alipotoka ndani na kuanza kukatiza katikati ya wanafunzi hao walimrushia chupa za mikojo na mifuko milaini yenye matope ndani yake.Machozi yalimtoka alijisikia vibaya sana kufanyiwa kitendo hicho na wanafunzi wake lakini kuna roho ilimwambia unastaili kufanyiwa ivo.

Alipelekwa moja kwa moja hadi rumande mpka uchunguzi kamili utakapo kamilika,polisi waliobaki waliwatuliza wanafunzi hao ili waweze kumsikilizA Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Bi.Mwamvita Abdallah.

Baada ya wiki moja kesi ya Profesa Maziku ilisikilizwa na Mahakama kuu ya mkoa Wa Dodoma ambapo Profesa Maziku alihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela bila Dhamana.Mke wake na watoto wake walilia sana kwasabab Profesa Maziku ndio alikua mtegemezi wao katika kila kitu.Wanachuo waliobahatika kuingia Mahakamani humo walishangilia mno na wale walio nje walishangilia pia baada ya wale walio ndani kutoka kwa shangwe.


Kwa kipindi hicho chote kabla kesi haijasikilizwa walikua washaletewa Profesa mwingne aliyeitwa Profesa Budongwa,masomo yaliendelea kama kawaida na Furaha ili rejea tena chuoni hapo ingawa wanachuo hao hawakuonyesha uaminifu Wa moja kwa moja kwa Profesa huyo.


..........................Itaendelea...............................................
Previous
Next Post »