Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini Mh. Vedasto Ngombale ameendelea na ziara mbalimbali katika jimbo analoliongoza.
ziara hizo ni muendelezo wa kutoa shukrani, kusikia na kujionea changamoto mbalimbali ambazo wananchi wamekua wakikumbana nazo kwa nia ya kuzitafutia ufumbuzi kama kiongozi ambaye ameaminiwa na wananchi wa jimbo la Kilwa Kaskazini.
kupitia ukurasa wake wa Facebook Mh. Ngombale ameandika ujumbe unaosomeka "Nimefanya mkutano na kamati ya maendeleo kata ya somanga kujadili namna ya kuanza ujenzi wa kituo cha afya. Nimeahidi kutoa mifuko 100 ya saruji na Tsh.5000000/= kutoka mfuko wa maendeleo ya jimbo."
kupitia ujumbe huo wachangiaji mbalimbali wameonyesha kuridhika na jitihada za Mheshimiwa kwa kumpongeza kwa jitihada zake ambazo anazionyesha katika kulisukuma gurudumu la maendeleo Kilwa Kaskazini na Nchi kwa ujumla.
mpaka sasa mbunge huyo amekwisha tembelea na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali ikiwemo kijiji cha Ingirito, kinywanyu, darajani, nandembo, miyumbu, mtyalambuko nk.
Sign up here with your email


ConversionConversion EmoticonEmoticon