Kilwa,
Kitendawili kilichokosa
jawabu Kwa muda mrefu hatimaye kimepata jawabu kwa kujulikana nani kusonga mbele na nani kuachia ngazi
katika mashindano ya Mshikamano Cup yanayoendelea kutimua vumbi katika mji Kingunge wa Kilwa kivinje.
Kitendawili hiko
kimeteguliwa baada ya kujulikana timu ambazo zinaungana na Black Mob Fc pamoja
na Kivinje soccer Academy katika hatua ya nusu fainali zinazotarajiwa kupigwa
tarehe 24 na 25 mwezi huu.
Mchezaji mwandamizi wa
Leicester City Fc Mustafa Makacho
ameendelea kuonyesha makali yake ya kucheka na nyavu za timu pinzani baada ya
kuisaidia timu yake kwa kuifungia goli 1 katika ushindi wa magoli 3 na kumfanya
kufikisha magoli 6 katika mashindano hayo.
![]() | ||
| Mustafa Makacho akiwa ameshika mpira wake aliokabidhiwa baada ya kufunga goli 3 katika moja ya mechi alizocheza katika Mshikamano Cup. |
Kwa matokeo hayo
Arsenal Fc, Leicester City Fc wanaungana na Black Mob Fc (Makuzi) na Kivinje
Soccer Academy katika hatua ya Nusu fainali inayoenda kuanza mapema siku ya
Alhamisi.
. RATIBA
KAMILI HATUA YA NUSU FAINALI MSHIKAMANO CUP.
_________________________________________
Tarehe: 24/08/2017
Mechi: Black
Mob Fc (Makuzi) V/s Kivinje Soccer Academy
Muda : Kuanzia
majira ya saa 10 jioni
Uwanja: Ukote
Stadium
Mahali: Kilwa
Kivinje
_________________________________________
Tarehe: 25/08/2017
Mechi: Arsenal Fc V/s Leicester City Fc
Muda : Kuanzia majira ya saa 10 jioni
Uwanja: Ukote Stadium
Mahali: Kilwa Kivinje
Mshikamano Cup ni ligi
ya mpira wa miguu iliyoanzishwa rasmi mwaka 2012 na hufanyika kila mwaka mwezi
wa 7 katika mji mkongwe wa Kilwa Kivinje katika uwanja wa Ukote, Ni mashindano
ambayo yamejizolea umaarufu mkubwa katika wilaya ya kilwa na viunga vyake kwa
kuibua vipaji, kujenga mshikamano miongoni mwa wapenzi wa kandanda sanjali na kutoa ajira kwa vijana.
Sign up here with your email

ConversionConversion EmoticonEmoticon