Kilwa,
Mbunge wa jimbo la
Kilwa kusini Mh. Selemani Bungara (Bwege) na msafara wake wamepata ajali katika
eneo la Migelegele.
Ajali hio imetokea
wakiwa safarini kuelekea kjiji cha Likawage ikiwa ni moja ya ziara za Mh. Bungara
za kutembelea vijiji ambavyo vipo ndani ya jimbo lake la kilwa kusini.
Kwa mujibu wa taarifa
za awali zinasema kua hakuna aliepoteza maisha katika ajali hio ila kuna baadhi
ya viongozi wamepata maumivu makali.
Chanzo kimesema
Mkurugenzi wa siasa Bw. Deo Chaurembo amepata maumivu makali ya ndani kwa ndani
na Katibu wa Mbunge Bw. Yusufu Saidi Abasi amepata maumivu kiasi huku Mh.
Selemani Bungara akiwa salama kabisa.
Majeruhi hao
wamefikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) kwa matibabu zaidi.
![]() | ||
| Bw. Yusufu Saidi Abasi akipata matibabu |
Uongozi wa
Mundunkolo.Blogspot unawapa pole ndugu zetu waliofikwa na ajali hiyo na mwenyezi
mungu awasimamie waweze kupona haraka ili waendelee na majukumu ya kulijenga
taifa.
Sign up here with your email


ConversionConversion EmoticonEmoticon