kilwa,
Kunani kilwa? Ndio
swali ambalo unaweza kujiuliza katika
fikra yako baada ya kusikia maajabu yanayoendelea kutokea
wilayani hapo.
Baada ya kuonekana
samaki mkubwa miezi kadhaa iliyopita akiwa amekufa katika eneo la masoko pwani,
wilaya ya kilwa hatimaye Ngisi mwenye ukubwa kuliko mazoea ameonekana maeneo hayo ya masoko pwani.
Kwa mujibu wa chanzo
chetu Ngisi huyo amekutwa anaelea akiwa amekufa ndipo akachukuliwa na kupelekwa
nchi kavu kama ilivyo ada.
Baada ya kukaguliwa na
wataalamu waligundua kua Ngisi huyo alikua amekufa siku za karibuni kwa kua
alikua hajaanza kuharibika sana na baadhi ya mikia yake ilikua imekatwa kwa
kuliwa na samaki baharini.
Baada ya kumpima alibainika
kua na kilo 23 na gramu 700 hali ambayo ilistaajabisha watu wengi kwakua ni nadra
sana kuona au kumpata Ngisi ambaye amezidi kilo 6 kwa sababu kwa kawaida Ngisi
mwenye kilo nyingi hufikia kilo 5 hadi 6.
![]() | ||
| Diwani kata ya Masoko Mh. Abuu Mussa Mjaka akiwa amemshika Ngisi ambaye ana kilo 23 na gram 700. |
Mundunkolo.Blogspot
ilitaka kujua ni sababu zipi zilizopelekea Ngisi huyo kua na kilo nyingi kuliko
mazoea? Swali ambalo lilijibiwa na Afisa uvuvi Wilaya ya Kilwa Bw. Mkali.
“Huyo Ngisi ni wa
kawaida kama ngisi wengine ila amefikia hatua hiyo kwa kua alikua anakaa kwenye
maji yenye kina kirefu, maji ambayo tofauti na yale ambayo wavuvi wanavuaga
Ngisi wengine
Kwahiyo alikua anakaa sehemu
ambazo ni mbali na maeneo ambayo wavuvi wa Ngisi wanafanya shughuli zao za
kiuvuvi hali ambayo imepelekea kuishi kwa muda mrefu na kukua mpaka kufikia
hatua hio” Alijibu
Amesema Ngisi huyo alisukumwa
na mawimbi ya maji baada ya kua amekufa ndipo Mvuvi aliemuona akamchukua.
Aidha Bw. Mkali
amewaambia wanainchi wasimtumie kwa chakula Ngisi huyo kwa kua bado
haijajulikana sababu iliopelekea kufa kwa Ngisi huyo.
Kwa sasa Ngisi huyo
anaonyeshwa kwa malipo ya Shilingi 500 kabla ya kufukiwa kwa kua hafai kwa
matumizi ya kibinaadamu (Kuliwa).
Sign up here with your email

ConversionConversion EmoticonEmoticon