MBUNGE WA KILWA KASKAZINI ATOA SHUKRANI KWA WANANCHI, AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO.



Kilwa,

Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini Mh. Vedasto Ngombale ametembelea katika kijiji cha Kinywanyu na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji hiko.


Katika mkutano huo uliohudhuriwa Na wananchi mbalimbali Mh. Ngombale aliwashukuru wananchi kwa kumuanini na kumpa kura zilizotosha kumpa ushindi wa kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


Aidha Mh. Ngombale alikagua majengo ya Shule pamoja na kutoa vifaa vya michezo kwa vijana kijijni hapo ikiwa ni jitihada za kuinua soka la wilaya ya Kilwa pamoja na ajira kwa vijana.


Kinywanyu ni moja ya vijiji ambavyo vinapatikana katika Jimbo la Kilwa Kaskazini ambalo linaongozwa na Mh. Vedasto Ngombale baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mh. Vedasto Ngombale akiwa katika ziara yake kijijini kinywanyu.







Previous
Next Post »