MKUU WA MKOA WA LINDI ATEMA CHECHE, ATOA AHADI YA KULA NAO SAHANI MOJA.

 Kilwa,

Mkuu wa mkoa wa lindi Mh. Godfrey Zambi amewataka watumishi kujiweka mbali na siasa pindi wanapo kua kazini.

Amesema ni haki ya kila mwananchi kuchagua chama ambacho anaona kinamfaa lakini ni marufuku kushabikia au kuleta uchama wanapokua kazi.

Mh. Zambi ameyasema hayo alipokua akiongea na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa katika ukumbi wa Jumba la maendeleo mjini kilwa masoko.

Amesema kuleta itikadi za uchama kazini kunaweza pelekea mpasuko baina ya watumishi wenye itikadi tofauti za kichama na kusababisha kazi kutoenda kama inavyotakiwa na kusababisha kuzolota kwa kazi na nchi kutoendelea.

“Kila mtu ana haki ya kuchagua na kukipenda chama ambacho anaona kwake kina mfaa, lakini si ruhusa kwa mtumishi kuleta ushabiki wa kichama sehemu za kazi” Alisema Mh. Zambi

Aidha Mh. Zambi amewataka watumishi kufuata sheria na kanuni za utumishi kwa kufuata yale walio amrishwa na kujiweka mbali na yale waliokatazwa kama watumishi wa umma.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa katika ukumbi wa Jumba la maendeleo 23.08.2017, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mh. christopher Ngubiagai kushoto ni Mkurugenzi mtendaji (W) Kilwa Bw. Zablon Bugingo.
Pia amaewatahadharisha watumishi ambao wanajihusisha na matumizi ya mitandao ya kijamii muda wa kazi na kuahidi kuwachukulia hatua kali pindi watakapobainika kwani wanakua hawa watendei haki watanzania ambao wanahitaji huduma kutoka kwao.

Baada ya kikao na watumishi Mh. Zambi alipata fursa ya kuzungumza na viongozi wa dini kutoka madhehebu mabalimbali, viongozi wa taasisi na wafanyabiashara kutoka wilayani kilwa.

Katika kikao hiko mheshimiwa Zambi amewataka viongozi wa dini na taasisi mbalimbali kutoa taarifa katika malmaka husika pindi wanapotaka kufanya mikutano au makongamano yao ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

Pia amewaomba viongozi hao kuhubiri amani na upendo katika nyumba za ibada na si vinginevyo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuendeleza amani na utulivu ambao watanzania wanajivunia kwa muda mrefu.
Previous
Next Post »