LECEISTER CITY FC YATINGA FAINALI, MAKACHO ATUPIA 2.



kilwa,
Mabingwa watetezi wa mashindano ya mshikamano cup Leceister city Fc kutoka yalipo makoa makuu ya wilaya ya kilwa wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali katika mashindano hayo  yanayofanyika kila mwaka kuanzia mwezi wa saba.

Leceister city wamafanikiwa kusonga mbele baada ya kuiadhibu timu ya Arsenal fc kutoka kilwa pande kwa goli 3 kwa 1 katika mchezo wa  nusu fainali uliochezwa  mapema  leo katika dimba la ukote.

Leceister city walikua wakwanza   kutikisa wavu wa  timu pinzani baada ya mshambuliaji wao machachali Mustafa Makacho jezi  namba 9 mgongoni kuwaandikia bao safi  la kuongoza dakika ya 9 ya mchezo  toka kuanza kwa mtanange huo.

Rashid Mtengula  aliiandikia Leceister City  goli la pili dakika ya 21 ya mchezo baada ya kuunganisha kwa shuti kali mpira  ulikua una ambaambaa baada ya kona iliyochongwa kutoka upande wa magharibi wa uwanja na kufanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa magoli 2 kwa 0 dhidi ya wapinzani wao.

kikosi cha Leceister city fc wakipasha misuli moto kabla ya mtanange wao na Arsenal Fc (picha na Ally Ruambo)

Mbaruku mbaruku akaifungia timu yake ya Arsenal bao la kufutia machozi dakika ya 53 kwa mkwaju wa penati  baada ya kufanyiwa madhambi akiwa katika kumi na nane ya timu pinzani.

Mustafa makacho akaendelea kua mwiba wa mashindano hayo bada ya kuzima matumaini ya mashabiki na wachezaji wa Arsenl Fc kutoka Pande kwa  Kutupia goli la 3 na la 2 kwake katika mchezo huo baada ya kutumia  vizuri makosa ya mlinda mlango wa Arsenal Fc Machejo Machejo katika dakika ya 88 na kumfanya afikishe  magoli 8 katika mashindano hayo.

Baada ya mtanange huo kuisha mchezaji Yahaya Maliki kutoka Arseanal Fc alichaguliwa kua mchezaji bora katika mpambao huo ulio isha kwa timu yao kufungwa goli 3 kwa 1.

Mchezaji wa Arsenal Fc Yahaya Maliki akipokea zawadi ya mchezaji bora wa mechi kati ya Arsenal na Leceister City.
Kwa matokeo hayo Leceister City itamenyana  na Black Mob Fc (makuzi) katika hatua ya  fainali ambayo inatarajiwa kupigwa juma mosi ya kwanza ya mwezi wa 9  ( tarehe 02/09/2017) katika dimba la ukote.

Black Mob Fc imetinga hatua ya nusu fainal baada ya kuitoa timu ya Kivinje Soccer Academy zote kutoka mjini Kivinje kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5 kwa 4 baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1 katika dakika 90 za mchezo.

Swali lililobaki vichwani mwa wapenzi wa soka wilayani kilwa na viunga vyake ni nani atachukua ubingwa wa mashindano ya mshikamano cup mwaka 2017? Je Leceister city watatea ubingwa wao au Black Mob Fc ( makuzi) watachukua kwa mara ya pili baada ya kuchukua ubingwa huo mwaka 2014?
 


Previous
Next Post »