Kilwa,
Hospitali ya wilaya ya
kilwa (kinyonga) imefanya mabadiliko kwa kutoka katika mfumo wa analogia na
kuhamia digitali katika utaratibu wa kusaini katika daftari la mahudhurio kwa
watumishi pamoja na mfumo wa kuhifadhi taarifa hospitali hapo.
Mabadiliko hayo
yamekuja siku chache baada ya kufungiwa mifumo maalumu ya kielektroniki ya
kuchukua taarifa za mahudhurio kwa watumishi kwa kutumia kifaa kijulikanacho
kwa jina la Biometrics Attendance Reader
pamoja na mfumo wa taifa wa kuhifadhi taarifa Hospitalini GoTHoMIS.
Biometrics attendence
reader ni kifaa cha kielekroniki chenye uwezo wa kurekodi na kutunza kumbukumbu
za mtumishi kuanzia jina, tarehe, saa, na dakika ambayo amesaini wakati wa
kuingia na kutoka kazini na mengineyo mengi baada ya kuweka alama ya kidole (finger print)
katika kifaa hiko.
GoTHoMIS ni mfumo ambao unahifadhi taarifa za
mgonjwa kielektroniki toka anaporipoti mapokezi mpaka mwisho anaepoenda
kuchukua dawa, bila kuhusisha matumizi ya daftrari kama awali.
Kupitia mfumo wa GoTHoMIS
taarifa za mgonjwa toka mapokezi zinatumwa moja kwa moja mpaka kwa Keshia
ambapo atalipia na kupatiwa risiti ambayo itamruhusu kwenda kuonana na
Daktari, ambapo atakuta baadhi ya taarifa zake za awali zimefika.
Baada ya kuonana na
Daktari maagizo yatakayotolewa na Daktari yatakua yame kwisha fika sehemu
husika ambayo mgonjwa ataelekezwa aende, kwa mfano kama atahitajika akapate
vipimo maabara, pumzishwe wodini, au apelekwe kwenye chumba cha upasuaji nk
taarifa zitakua zimesha fika sehemu husika.
Baada ya kumaliza matibabu
kumbukumbu za mgonjwa zitabaki katika mfumo huo uliofungwa hospitali hapo na
iwapo atarudi kwa siku nyingine atataja jina lake tu,na taarifa zake za awali zitaonekana kabla ya kuendelea na matibabu.
Kupitia mifumo hio
mipya uongozi utapata kuona na kujua orodha ya watumishi ambao ni watoro
kazini, wanaochelewa kufika na wanao wahi kutoka kabla ya muda uliopangwa
pamoja na kuwa na kumbukumbu sahihi za taarifa za wagonjwa, matumizi ya dawa pamoja
mapato ya kila siku hospitalini hapo.
Picha ya Biometrics Attendance Reader, kifaa kinacho tumika kuchukua taarifa za mahudhurio kwa watumishi kwa kutumia alama ya kidole.
Akionyesha kufurahishwa
na mifumo hio mipya Katibu wa afya Hospitali ya wilaya Kinyonga Bi. Zabibu Uledi amesema mifumo hio mipya
itasaidia sana kurahisisha upatikanaji wa takwimu za mahudhurio ya watumishi,
wagonjwa na kumbukumbu zingine kwa haraka sana ukifananisha na mifumo iliokua
ukitumika awali.
Aidha Bi. Zabibu amewaomba watumishi watumie
mifumo hio kwa umakini na uangalifu ili iweze kudumu kwa muda mrefu na hatimae kuleta
matokeo chanya.
“Ni waombe tu watumishi
wawe waangalifu kwenye utumiaji wa mifumo hii ili iweze kudumu kwa muda mrefu.”
alisisitiza.
Nae Bi.Veronica akizungumza kwa niaba ya
watumishi wengine wa hospitali ya kinyonga amesema wanashukuru kwa mifumo hio mipya kwani ni
mizuri na itasaidia kuondoa msongamano muda wa kusaini kwa kua mfumo huo
unafanya kazi kielektroniki zaidi pia mfumo wa GoTHoMIS utasaidia
upatikanaji wa kumbukumbu sahihi za wagonjwa hospitalini hapo.
Mfumo wa kielektroniki
wa GoTHoMIS umekwisha anza kutumika
hospitali hapo majuma kadhaa yaliyopita licha ya kukumbwa na changamoto kubwa
ya baadhi ya watumishi hospitali hapo kutokua na ujuzi wa kutumia kompyuta
wakati mfumo kusaini kwa kutumia alama za vidole (finger print) unatarajiwa
kuanza kutumika siku chache zijazo.
Hospitali ya kinyonga
ni taasisi ya pili kunufaika na mfumo huo wa kidigitali wa kuchukua taarifa za
mahudhurio kwa watumishi baada ya idara mbalimbali zilizopo katika makao makuu
ya halmashauri ya wilaya ya kilwa kunufaika na mfumo huo.
Halmashauri ya wilaya
ya kilwa ni miongoni mwa wilaya chache Tanzania ambazo zinatumia mfumo wa kidigitali wa kuchukua
rekodi za mahudhurio kwa watumishi wake pamoja mfumo wa taifa wa kuhifadhi
taarifa Hospitalini (GoTHoMIS).
Sign up here with your email

ConversionConversion EmoticonEmoticon