Kilwa,
Jeshi la polisi wilaya ya kilwa
linawashikilia watu zaidi ya 30 kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za uvuvi
kinyume na sheria.
Wavuvi hao wamekamatwa Jana
katika operesheni maalum ambayo iliongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wilaya kilwa Mh. Christopher
Ngubiagai katika kambi ya wavuvi hao inayojulikana kwa jina la Msangamla, Kilwa Kisiwani.
Operesheni hio imekuja
baada ya kupokea malalmiko kutoka kwa wanainchi juu ya ukiukwaji wa sheria
uliokua unaendelea katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na uvuvi usiofuata sheria,
matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bhangi.
Akizungumza na
mwandishi wetu Afisa uvuvi wilaya ya kilwa Bw.Hussein Rambo amesema wameamua
kufanya oparesheni hio ikiwa ni njia moja wapo ya kuthibiti Wavuvi wahamiaji
ambao wanavua bila yakua na vibali kutoka mamlaka husika pamoja na kupunguza
wimbi la vitendo vya uvuvi haramu.
Amesema kwa yeyote
anayetaka kuendesha shughuli za uvuvi wilayani kilwa anakaribishwa, lakini
afuate sheria na kanuni kama baadhi ya wavuvi kutoka sehemu mbalimbali nje ya
kilwa walivyofanya.
“Tunamkaribisha mtu
yeyote kuja kufanya shughuli za uvuvi wilayani kilwa ila afuate sheria ambazo
zimewekwa “alisema
Bw. Rambo amesema ili
uweze kutambulika na kufanya shughuli za uvuvi wa kuweka makazi (Dago) wilayani
kilwa na viunga vyake inabidi ufuate misingi ya sheria kwa kufanya mambo kadhaa
ikiwemo:-
Mosi, mvuvi inabidi awe
na barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa uvuvi ambako mvuvi anatoka ikiwa imeambatanisha
na Leseni ya Uvuvi.
Pili, Muombaji atawasilisha
vielelezo hivyo , na baadae atakutana na Bmu ya sehemu husika ambapo
watamjadili pamoja na kukagua zana zake za kazi kama zinaendana na sheria na
kanuni za uvuvi, baada ya Bmu kuridhia Mwombaji ataonana na Afisa Uvuvi wa
wilaya na kupatiwa Kibali cha kuendesha shughuli za uvuvi ambacho kitadumu kwa
muda wa miezi mitatu.
Baada ya miezi mitatu
kupita Mvuvi ataenda kwa Afisa uvuvi kwa ajili ya kupewa tena Kibali kama
atahitaji kuendelea na shughuli za uvuvi.
watuhumiwa wakiingia katika gari
Akikanusha shutuma juu
ya tukio hilo Bw. Rambo amesema sio kweli kwamba wakazi wa Kilwa Kisiwani
hawataki Wavuvi wahamiaji bali ni utaratibu ambao upo na unatumika si Kilwa
Kisiwani tu bali hata sehemu zingine.
“Sio kweli kwamba
wakazi wa Kilwa Kisiwani hawataki wavuvi kutoka nje ya kitongoji chao bali ni
utaratibu ambao upo kwamba , inabidi uwe na vibali ambavyo vinakutambulisha kua
wewe ni nani na umetekea wapi kwa sababu
za kiusalama zaidi”. aliongeza
Aidha Bw. Rambo
amewashauri wanainchi wa Kilwa na kutoka nje ya Kilwa kufuata sheria ili
kuepukana na mkono wa sheria.
Katika operesheni hio
ilioendeshwa na kamati ya ulinzi na usalama , maafisa uvuvi, Bmu pamoja na
baadhi ya viongozi kutoka katika kitongoji hiko nyavu za kioo (monofilament
net) pamoja na Mabanda kadhaa ambayo yalikua yanatumiwa na wavuvi hao
yameteketezwa kwa moto .
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon