HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA YAIKABIDHI TARURA MIRADI YA BARABARA.



Kilwa,         
            Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Nd. Zablon Bugingo amekabidhi miradi ya barabara Kwa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilwa Mhandisi Respicius Matungwa.

Makabadhiano hayo yamefanyika mapema leo tarehe 31.08.2017 katika ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kilwa Mh. Abuu Mussa Mjaka, Mwanasheria wa Halmashauri Bw. Yusuf Msosa   na aliyekua  Mhandisi wa Halmashauri Nd. Chande.

Hatua hio imefikiwa ikiwa Ni utekelezaji wa agizo la serikali la kubadili usimamizi wa miradi ya Barabara kutoka katika Mamlaka za serikali za mitaa kwenda kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA).

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndugu.Zablon I.Bugingo (Katikati)  akimkabidhi miradi ya Barabara  Meneja wa TARURA Wilaya ya Kilwa  Eng.Respicius C. Matungwa  kutoka kulia ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Yusufu Msosa, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Abuu Mussa Mjaka.


Akitoa shukrani zake za dhati baada ya kukamilika wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Nd. Zablon Bugingo amesema anashukuru sana kwa kufanikisha makabidhiano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa Wakala huyo .

TARURA( Tanzania Rural and Urban Agency) ni wakala wa Barabara wa za vijijini na mijini Tanzania ambaye ameanzishwa rasmi  kwa dhumuni la kusimamia shughuli zote zinazohusiana na Barabara ambazo awali zilikua zikifanywa na Mamlaka za serikali za mitaa.


Previous
Next Post »

2 comments

Write comments
Unknown
AUTHOR
31 August 2017 at 19:24 delete

Upo vizuri kiuandishi waitendea haki kalamu yako mungu Akuongoze

Reply
avatar