Kilwa,
Basi mali ya kampuni ya Ibra Express inayofanya
safari zake kati ya Dar es salaam na Masasi limeteketea kwa moto.
Mkasa huo umetokea jana maeneo ya Nangurukuru
Wilayani Kilwa takribani kilomita 2 kutoka Nangurukuru mjini.
Basi hilo lilikuwa linatokea jijini Dar es salaam kuelekea Mjini Masasi.
Basi hilo lilikuwa linatokea jijini Dar es salaam kuelekea Mjini Masasi.
![]() | ||
| Basi - Ibra Express likiwa linawaka moto |
Taarifa za awali kutoka katika chanzo chetu zinasema hakuna aliyepoteza maisha
wala kupata majeraha katika mkasa huo.
Mpaka habari hii inatoka chanzo cha moto uliopelekea
kuteketea kwa Basi hilo bado kilikua hakijafahamika, huku mashuhuda wakidai wenda hitilafu katika mfumo wa umeme katika basi hio ndio umepelekea gari hio
kuteketea kwa moto.
Sign up here with your email


ConversionConversion EmoticonEmoticon