Kilwa,
Timu ya sevilla fc kutoka
kilwa masoko imekubali kipigo cha goli mbili kwa nunge kutoka kwa ndugu zao wa
Kilwa Youth Soccer Academy kabla ya mpambano huo kukatishwa kwa vurugu.
Wachezaji wa kilwa youth soccer academy wakiwa
mbele kwa goli 2 kwa bila wali amrishwa kutoka nje ya uwanja baada ya mchezaji mwenzao
kuchezewa madhambi.
Samuel Galafao mwalimu
wa Kilwa Youth Soccer Academy alikiamuru kikosi chake kitoke uwanjani kwa kile
alichodai kuwa walikua wanachezewa michezo isiyokua ya kiungwana hali ambayo
ilikua iki hatarisha afya ya wachezaji wake licha ya kutoa onyo mara kadhaa.
Mchezo huo wa kirafiki umepigwa mapema leo katika uwanja
wa Mwenge (Taifa) mjini kilwa masoko ikiwa ni mchezo wa kujipima nguvu kwa timu hizo pamoja na kusindikiza sherehe za sikukuu ya iddi elhaji ambayo imesherehekewa leo duniani
kote.
![]() | |
| kiranja wa Sevilla Fc Selemen Charahani (Kushoto) akichuana na Juma Mbaga katika mechi ya kirafiki ilioisha kwa Kilwa Youth Soccer Academy kuibuka na ushindi wa goli 2 kwa 0 (picha na Ally Ruambo) |
Mohamedi Hafidhi ndie
aliye anza kutikisa wavu wa sevilla Fc baada ya pasi za hapa na pale, goli
ambalo lilidumu mpaka mwamuzi alipopuliza kipyenga cha mapumziko.
Kipindi cha pili
kilionyesha mabadiliko kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu kabla ya Juma Mandai (Kaseja) kuitimisha kalamu ya magoli kwa kuipachikia
timu yake Kilwa Youth Soccer Academy goli
ambalo lilidumu mpaka pale mpambano huo ulipokatishwa kutokana na vurugu zilizo
jitokeza.
Baada ya mtanange huo
kuvunjika wadau mbali mbali wa soka walimtaka Kiongozi wa Sevilla Fc kuongea
na wachezaji wake juu ya swala zima la nidhamu pamoja na kucheza michezo ya
kiungwana kwani mchezo wa soka ni
wa amani na sio uadui.
Kwa upande wake
kiongozi wa Sevilla Fc alikubali na kuomba msamaha kwa niaba ya timu yake na kuahidi kua matukio kama hayo hayatojitokeza tena.
Sign up here with your email


ConversionConversion EmoticonEmoticon